Kamanda Muliro Athibitisha Dr Slaa Akamatwa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha kukamatwa kwa Dk. Willibrod Peter Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Karatu na pia Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

“Ni sahihi daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya naamini taarifa zaidi zitatolewa baadaye,” amesema.

Dk. Slaa alikamatwa usiku wa kuamkia Januari 10, 2025, nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam. Sababu za kukamatwa kwake bado hazijawekwa wazi, lakini mahojiano yanaendelea vizuri kuhusu mambo kadhaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii