Naibu Katibu mkuu wizara ya
maji ,Mhandisi Nadhifa Kemikimba ametembelea mradi wa maji wilayani
Longido na kusema wameridhishwa na mradi huo unavyotekelezwa.
Aliyasema
hayo wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji wilayani Longido
unaotekelezwa na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira jiji la
Arusha (AUWSA)huku akifuatana na Mkurugenzi mtendaji wa benki ya
maendeleo ya Afrika katika kujionea miradi hiyo ilipofikia na maendeleo
yake.
"Kwa kweli tumefurahishwa Sana na ugeni wa Mkurugenzi
mtendaji wa benki hi ambao wameweza kuridhishwa na matumizi ya fedha
tulizotumia katika mradi huu, na kuwa fedha tulizopewa hatujazifanyia
mchezo na hakuna mahali tumechelewesha tangu kuanza kwa mradi
huu."alisema .
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo ya
Afrika ,Amos Cheptoo ameeleza kuridhishwa na serikali ya Tanzania katika
usimamizi wa matumizi ya fedha hizo zilizotolewa na benki hiyo
kutekeleza mradi mkubwa wa maji jijini la Arusha na maeneo jirani .
"Naipongeza sana serikali kupitia wizara ya maji pamoja na AUWSA kwa namna ambavyo wameweza kuwekeza katika.sekta ya maji kwa kutekeleza mradi huo kwa umakini na uaminifu mkubwa ambapo mradi huo ukikamilika utaweza kuwanufaisha wananchi wengi na kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji na hatimaye kuweza kupunguza maradhi yatokanayo na ukosefu wa maji kwa ujumla."alisema.
Naye Mkurugenzi wa AUWSA jiji la
Arusha,Mhandisi Justine Rujomba alisema kuwa,hivi Sasa wameshakamilisha
zoezi la mfumo wa majitaka na kinachofanyika Sasa hivi ni ulazaji wa
mabomba ya maji Safi na kuwa mradi huo umeweza kupunguza makali ya mgao
wa maji .
Mhandisi Rujomba alisema kuwa,hapo awali walikuwa
wanapata kiwango cha maji Lita milioni 40 kwa siku ambapo kwa Sasa hivi
wanapata kiwango cha lita milioni 60 kwa siku ,hivyo kuondoa kabisa
changamoto ya mgao wa maji