Sauti za Busara Yatoa Orodha ya Wasanii kwa Tamasha la 2025

Waandaji wa Tamasha la Sauti za Busara, linalofanyika visiwani Zanzibar kila Februari, wametangaza orodha ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la 22, litakalofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 16 Februari 2025.

Tamasha hili linakusanya bendi maarufu na zinazochipukia kutoka kanda zote za Bara la Afrika, likiongozwa na msanii nguli wa muziki kama Thandiswa (South Africa), Blinky Bill (Kenya), Christian Bella & Malaika Band (Tanzania), Bokani Dyer (South Africa), Frida Amani (Tanzania) ,Wura Samba (Nigeria), The Zawose Queens (TZ/UK), Kasiva Mutua (Kenya), Zanzibar Taarab Heritage Ensemble (Zanzibar), Leo Mkanyia & Swahili Blues (Tanzania, Boukouru (Rwanda), Tryphon Evarist (Zanzibar, Charles Obina (Uganda), Baba Kash (Tanzania) Anna Kattoa & Bantu Sound (Zanzibar)

Wasanii wengine watakaoshiriki ni pamoja na Tarabband (Sweden), Assa Matusse (Mozambique), Mumba Yachi (Congo),Nidhal Yahyaoui (Tunisia) ),Étinsel Maloya (Reunion),WD Abo (Sudan) B.Junior (Mayotte), uKhoiKhoi (South Africa),Joyce Babatunde (Cameroon) na wengine.

 

Kaulimbiu ya tamasha lijalo ni "Amani Ndiyo Mpango Mzima." akielezea kuhusiana na orodha ya wasanii na alama ya tamasha hili, mkurugenzi wa tamasha Journey Ramadhan anaeleza, “Tamasha linaangazia ubora na muziki wa aina mbalimbali kutoka kote barani Afrika, hasa wanamuziki wa kike, chipukizi wenye sauti za kipekee, jumbe zenye nguvu, na zinazoleta mabadiliko chanya kwa jamii, Kwa wazanzibari, tamasha hili ni fursa ya kuonyesha utamaduni wao adhimu, kuimarisha utambulisho wa kitaifa, amani, umoja, na kuhamasisha vijana kujivunia urithi wao.Kwa Waafrika kwa ujumla, ni jukwaa la kusherehekea ufanisi wa sanaa na muziki wa Kiafrika, kuimarisha mahusiano kati ya mataifa, na kuhamasisha mabadiliko chanya kupitia sanaa.”

Tamasha hili limekuwa jukwaa linatoa nafasi kwa wasanii wapya kujitokeza na kuonyesha vipaji vyao, huku wakiongeza wigo wa soko lao na kuungana na wasanii wengine ndani na nje ya Afrika. Hii ni fursa ya kipekee ya kukuza sanaa zao.

 

Wanaotembelea tovuti yetu wanaweza kutazama video na kujua zaidi kuhusu vikundi vyote vitakavyotumbuiza Februari 2025 katika toleo hili la 22.

 

Tamasha la 22 litafanyika Zanzibar, kuanzia tarehe 14 – 16 Februari 2025. Kiingilio kwa Watanzania ni shilingi 40,000/- kwa tiketi za kawaida za siku tatu, au 20,000/- kwa tiketi ya siku moja.

 Tiketi za mapema zinapatikana mtandaoni kupitia jukwaa la Tukiio na kwenye tovuti yetu ya Sauti za Busara.

Sauti za Busara 2025 inawezeshwa na Fumba Town, mradi wa CPS; Zanlink, na wengineo watakaothibitishwa baadaye.

Kwa maelezo zaidi: www.busaramusic.org

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii