Dikembe Mutombo, nyota wa mpira wa kikapu na mchezaji nguli wa NBA afariki

Alikuwa mchezaji nguli wa NBA, na si kwa umbo tu. Dikembe Mutombo, mchezaji nguli wa mpira wa vikapu kwa misimu 18 katika NBA, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 siku ya Jumatatu, Septemba 30. 


Aliugua saratani ya ubongo. Beki bora mara nne katika ligi ya Amerika Kaskazini, maarufu kwa uchezaji wake mkali na vitendo vyake vya kibinadamu, mzaliwa huyo wa Kongo umaarufu wake kwenye mchezo wake na kwingineko, haswa barani Afrika na DRC.

Mutombo aliaga dunia akiwa amezungukwa na familia yake baada ya kuugua saratani ya ubongo. Kamishna wa NBA Adam Silber amesema uwanjani Dikembe Mutombo alikuwa miongoni mwa walinzi bora aliyezuia mipira katika historia ya NBA na nje ya uwanja alikuwa na moyo wa kuwasaidia watu wengine.

Na kusema kwamba awali alikusudia kuwa daktari… “Doc’ Mutombo” au “Prof’ Mutombo” ingesikika vizuri. Alipowasili Marekani mwishoni mwa miaka ya 1980, Dikembe Mutombo, mwanariadha mahiri aliyefikia kilele cha mita 2.18, alipendelea mpira wa chungwa kuliko stethoscope. Na hivi ndivyo alianza kujipatia umaarufu.

Daktari mwanafunzi ambaye alikua mchezaji wa mpira wa kikapu

Dikembe Mutombo Mpolondo Mukamba Jean-Jacques Wamutombo - jina lake kamili - alizaliwa Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Juni 25, 1966, ndani ya familia kubwa ya kabila la Luba.

Hatima ya mwanafunzi huyu mwenye bidii – haishangazi, akiwa na baba ambaye alikuwa mkuu wa shule na kisha afisa mkuu katika Elimu.

Mutombo, ambaye alicheza kwa misimu 18 katika ligi ya NBA alifanya juhudi kubwa kuboresha hali ya maisha katika nchi yake alikozaliwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia wakfu wake binafsi.

Dikembe Mutombo alistaafu NBA mnamo mwaka 2009 baada ya kuchezea timu kadhaa zikiwamo Denver Nuggets, Atlanta Hawks, Philadelphia, New Jersey Nets, New York Knicks na Houston Rockets.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii