Maandamano mapya Oktoba Mosi, Polisi watoa tamko

Sehemu ya raia wa Nigeria wametangaza nia yao ya kufanya maandamano siku ya Jumanne, Oktoba 1, wakati taifa hilo la Afrika Magharibi litakapokuwa likiadhimisha miaka 64 ya uhuru wake.

Mratibu wa kitaifa wa vuguvugu la Vijana wa Nigeria, Juwon Sanyaolu amesema maandamano hayo wameyapa jina la #FearlessOctober1 na na yatafanyika nchini kote, kushinikiza kurejeshwa kwa ruzuku ya mafuta na ushughulikiaji wa mapungufu ya kiuchumi.

Amesema, tayari wamewafahamisha Polisi kuhusu maandamano hayo yaliyopangwa na wanatarajia kukutana katika uwanja wa Eagle Square katika mji mkuu Abuja, na chini ya darajala Ikeja katika jiji la kibiashara la Lagos.

“Tumemwandikia inspekta mkuu wa polisi kumfahamisha kuhusu maeneo yetu ya maandamano,” Sanyaolu alisema, kama alivyonukuliwa na gazeti la Punch la Nigeria,” alisema Sanyaolu.

Kufuatia taarifa hiyo, Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nigeria, Kayode Egbetokun ameamuru kutumwa kwa maafisa wa Polisi katika vituo vya kimkakati vya Serikali, ili kuwalinda dhidi ya uharibifu unaoweza kutokea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii