Mwanajeshi apandishwa cheo kwa kumsaidia mwanamke kujifungua Zambia

Mwanjeshi wa Zambia amepandishwa cheo cha kijeshi kwa kumsaidia mwanamke mjamzito kujifungua mtoto katika shamba la mahindi.

Humphrey Mangisani amepadishwa cheo kutoka askari alisiye na cheo hadi kopro kamili kwa ujasiri wake.

Tukio la kuzaliwa kwa mtoto huyo, ambayo kwa mujibu wa taarifa kutoka Zambia - - lilitokea wiki iliyopita katika wilaya ya mashariki mwa nchi ya Petauke, ilijulikana kote nchini.

Kopro Mangisani alisema aliitwa kumsaidia mwanamke huyo ambaye alikuwa amepata uchungu wa uzazi.

Alimtafutia pikipiki ya bodaboda ambayo ilimpeleka hospitali na kumfuata nyuma na bodaboda nyingine ili kufuatilia hali yake.

Lakini uchungu wake ulikuwa wa haraka kiasi kwamba walilazimika kuweka kando pikipiki na kumsaidia kujifungua mtot mchanga katika shamba moja la mahindi lililopo kando ya barabara.

“Nilitafuta na kupata wembe haraka na kumsaidia kukata kitovu. Mvua ilikuwa inanyesha alipojifungua. Nikamchukua mtoto haraka nikampeleka hospitalini na mama yake akafuata nyuma," alisema.

Askari huyo alikabiliwa na adhabu kwasababu ilibidi asiwepo kambini bila likizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii