Mwanamke Mrwanda, Mukandamage Domitila aliwashtua wengi baada ya kufichua alikuwa ameolewa na ndugu yake wa damu moja.
Domitila alizaliwa mnamo mwaka 1978, lakini mwaka mmoja baadaye mama yake alifariki dunia.
Kisha miaka michache baadaye alimpoteza baba yake na hivyo alikuwa na ndugu wengi ambao walikulia katika familia tofauti.
Katu hakuwa anamfahamu kaka yake japo jamaa zake walikuwa wakimuarifu kwamba ana kaka.
Baada ya miaka mingi, Domitila alianza kufanya kazi kama kijakazi na siku moja alikutana na kaka yake jijini Kigali, Rwanda, lakini hawakujua wao ni watu wa damu moja.
Ndugu hao walipendana sana na kisha walioana na kujaliwa watoto watatu.
Baadaye waligundua kwamba wao ni ndugu wa damu moja waliotoka tumbo moja na baba yao ni mmoja.
Taarifa hiyo ilimuhudhunisha Domitila na kumfanya kujidharau sana akijifungia akijificha kukutana na watu.
"Nilichanganyikiwa na kuanza kujificha kwa watu. Niliacha hata kuchota maji..." alisema domitila.
Domitila alisema watu walikuwa wamdhihaki pamoja na wanawe wakisema walizaliwa na damu moja na hivyo kumlazimu kutengana na kaka yake.
Mama huyo anaishi katika nyumba mbovu ambayo haijamalizwa kujengwa na hapokei msaada wowote kutoka kwa baba ya watoto wake.
Kifungua mimba wa Domitilia na mwanawe wa pili wana matatizo tofauti za kiafya.
Domitila alisema ni miaka mitano sasa tangu atengane na kaka yake ambaye hataki kujihusisha na wanao.
Anawaomba wasamaria wema kumsaidia kujenga nyumba mpya kwa ajili ya familia yake na kuwapeleka watoto wake shuleni.