Maporomoko ya ardhi yaua takriban watu 229 kusini mwa Ethiopia

Takriban watu 229 walifaiki katika maporomoko ya ardhi, tukio lililotokea Julai 22 kusini mwa Ethiopia baada ya mvua kubwa kunyesha, kulingana na ripoti ya muda ambapo idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi, mamlaka za ndani zilitangaza Julai 23, 2024.

Kutoka 55, idadi ya watu iliongezeka hadi 146, kisha angalau wahanga 229 katika mkasa wa Geze-Gofa, kusini mwa Ethiopia. Maporomoko makubwa ya ardhi yalitokea hapo Julai 22, 2024. "Taarifa iliyotolewa kufikia sasa inaonyesha wanaume 148 na wanawake 81, au jumla ya watu 229 waliopoteza maisha" katika janga hili, inaonyesha huduma ya mawasiliano ya eneo la utawala la Gofa, abapo tukio hilo lilitokea.


Maelezo machache yanapatikana kuhusu maafa haya yaliyotokea katika eneo la mashambani, lenye milima na lililotengwa, zaidi ya kilomita 450 kwa saa kumi kwa kutembea gari kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa, katika wilaya ya Geze-Gofa.


Picha zilizorushwa na mamlaka za ndani na vyombo vya habari vya Ethiopia zinaonyesha maporomoko makubwa ya matope. Sehemu nzima ya kilima imetengwa. Walionusurika hujaribu kutoa miili iliyosombwa kwa kutumia zana za muda au wakati mwingine hata kwa mikono yao mitupu. Wengi wa waathiriwa walisombwa na tope hilo walipokuwa wakijaribu kuwasaidia wakazi wengine.


Jimbo la Kanda ya Kusini mwa Ethiopia ni miongoni mwa maeneo mengi ambayo yaliathiriwa na mafuriko kote nchini mwezi Aprili na Mei wakati wa msimu mfupi wa mvua. Muda mrefu, ulianza mwezi Juni katika nchi hii ya Afrika Mashariki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii