TIC YAWAHIMIZA WATANZANIA KUWEKEZA NA KUJISAJILI

WATANZANIA wanaotamani na waliowekeza Nchini wamehimizwa kwenda kujisajili katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwani kuna manufaa makubwa ya kujisajili katika kituo hicho.

Mwekezaji Mtanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kutengeneza gundi kilichopo Nyakato Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Kapocha Makongoro baada ya kupokea ugeni kutoka makao makuu ya kituo hicho uliokua na lengo la kujionea maendeleo ya kiwanda hicho kinachomilikiwa na mtanzani.

Kapocha ameeleza kuwa kuna faida nyigi za kujisajili TIC mojawapo ni kupata gharama nafuu ya uagizaji wa bidhaa mbalimbali na ikiwemo mitambo na kupata fursa mbalimbali kutoka TIC.

Kwa upande wake Meneja wa SIDO Mkoa wa Mwanza Bakari Songwe amesema kuwa lengo la SIDO ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wadogo wanakua na bidhaa zinazofika sokoni kwa kushirikiana na serikali, wawekezaji na wadau wengine wa maendeleo



Mkurugenzi wa wa utawala na fedha wa kituo cha uwekezaji TIC Paschal Maganga amesema kuwa lengo kubwa la kufika Jijini Mwanza ni kuhakikisha wahamasishe uwekezaji wa ndani ikiwemo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani ambae amefungua Nchi katika uwekezaji.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii