Msanii wa muziki wa injili ambaye anawakilisha nchini Rwanda Alpha Rwirangira Tunamfahamu kwa kazi zake nyingi ambayo amewahi kuzifanya na kukonga nyonyo za mashabiki zake mbali mbali kutokana na upekee wa sauti yake na ujumbe ambao amekuwa akiwasilisha kupitia talanta yake.
Alpha baada ya kukaa kimya kwa takribani mwaka mmoja ameamua kuachia wimbo wake mpya alioupatia jina la I’M FREE wimbo ambao una ujumbe mzuri ndani yake ukiwa na video ambayo imeongozwa na muongozaji maarufu kwa jina la Kavoma.
Ujio huu ni wa kipekee kwa Alpha ambaye anaamini unaweza kuutumia katika nyakati mbali mbali kusheherekea harusi,siku ya kuzaliwa na mengine mazuri.
Wimbo unapatikana katika vyanzo vyote vya kupakua na kusikiliza muziki .