ROBY TONE ANASEMA BAADA YA SIRI SASA NI NAKUGANDA

Tanzania imebarikiwa vipaji vingi ,na kila siku kuna wasanii wapya wanaibuka katika kulisukuma gurudumu la muziki Tanzania kama inavyoaminika kuwa muziki ni biashara ulimwenguni ndivyo ambavyo wasanii wengi wameshindwa kupata usingizi ili kufanya mbinu za kibunifu katika harakati za kuifanya biashara hiyo ya muziki kuwa yenye faida kwao.