RICH MAVOKO KUFANYA ALBUM NDIO UKUBWA WA MSANII NITATOA NYINGINE.

Rich mavoko ambaye mwaka huu tangu uanze nyimbo alizoachia ni tatu yaani miss you,my g na sasa ni kill myself akiwa ameshirikiana na chino kid moja ya msanii ambaye kwake ni kama mdogo wake lakini pia anapenda uwezo wake na ulifika muda muafaka wa wao kufanya kazi ndio maana kazi hiyo ikatoka.

 

Akizungumza na Mtangazaji Natty e Brandy Pamoja na B 45 kupitia kipindi cha Hitzone Mavoko aliulizwa kipi ambacho alijifunza  katika utoaji wa album ambacho labda alikidhani na ikawa ndivyo sivyo na akasema “Nilichojifunza unapotoa album kwa sababu ni mtiririko wa nyimbo nyingi ni lazima uwe na matangazo yakutosha n ani kitu nilijifunza kupitia album yangu ya fundi ambayo ni kubwa sana”Alisema mavoko na kuongeza kuwa ili uwe msanii kamilifu ni lazima uwe umetoa album kwa hiyo tegemeeni album nyingine.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii