Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wanawake na Makundi Maaum, Dkt. Dorothy Gwajima, amepokea ugeni wa
Shirika la kupigania haki za wananawake na usawa wa kijinsia katika
nafasi za uongozi, UN Women, na kuweka mikakati ya pamoja katika kufanya
kazi na kuwahudumia wanatanzania katika masuala ya usawa wa kijinsia.
Ugeni
huo kutoka UN Women, ukiwa umeongozwa na Mwakilishi Mkaazi, Hodan Addou
pamoja na Mkuu wa masuala ya maendeleo kutoka nchini Finland Timo
Voipio, ulimuelezea Waziri Gwajima, dhamira ya Shirika hilo, kusaidiana
na Serikali katika msuala ya usawa wa kijinsia kwenye uongozi hususan ni
ngazi za jamii kwenye Serikali za Mitaa.
Akizungumza katika
kikao hicho Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameuambia ujumbe huo kuwa, kama Wizara wapo
tayari kufanya kazi na shirika hilo hasa kwa upande wa vipaumbele ambayo
Wizara imejiwekea ikiwepo kukuza usawa wa kijinsia kwa viongozi katika
ngazi jamii ambapo tatizo limeoneka kuwa kubwa ikilinganishwa katika
ngazi ya Mikoa na Taifa.
Dkt. Gwajima ameongeza kuwa kwa sasa
Wizara inaandaa taarifa ambayo itawasilishwa nchini Marekani kwenye
Umoja wa Mataifa, ambapo taarifa hiyo itaangazia athari za hali ya
mabadiliko ya tabia nchi na kwa namna gani wanawake wa watanzania
wamejipanga kupambana na hali ya mabadiliko ya nchi sambamba na masuala
ya uongozi na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi.
“Chini
ya Uongozi wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tumepiga hatua kwa nafasi
za wanawake ngazi za juu, lakini kama Wizara tunataka elimu hiyo, ifike
ngazi za jamii ambako bado uelewa bado upo chini, hivyo kupitia Shirika
lenu la UN Women tunaimani tutafanikiwa katika hili” alisema Dkt.
Gwajima.
Kwa upande wake Meneja wa Programu katika kuwainua
wanawake, Lilian Mwamdanga, kutoka Un Women, aliyekuwa ameambatana
katika ujumbe huo, amesema pamoja na mambo mengine yakuangalia usawa wa
kijinsia vilevile wataona namna gani nzuri yakushirikiana na Serikali
katika kuangalia baadhi ya Sheria na miongozo.
“Kwakuwa hii ni
Wizara mpya na Mhe. Waziri umetuelezea uwepo wa baadhi ya Sera
zinazomzungumzia mwanamke au mambo ya usawa wa kijinsia lakini kwa namna
moja au nyingine zimepitwa na wakati na zingine zipo lakini utekelezaji
wake una sura ya kusua sua, hivyo UN Women, tupo tayari kusaidiana
kuandaa miongozo mipya itakayokwenda na wakati, amesema Liliani.
Pamoja
na mambo mengine Shirika hilo la limeahidi kuandaa Semina ndogo kwa
viongozi ili kuwapitisha viongozi na watendaji kuweza kupambanua
shughuli zao wanazo zifanya hapa nchini kama UN Women ili viongozi na
watendaji waseriali waweze kuona fursa zaidi walizonazo.
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, imeendelea
kupokea wadau mbalimbali wa maendeleo itakaoshirikiana nao katika
kutekeleza afua mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara hiyo.