Wadau wa soka Tanzania wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya raundi ya pili ya mechi za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wikendi hii, kwa hisani ya Guinness, Bia Rasmi na Bia Rasmi Isiyo na Kilevi. Serengeti Breweries Limited (SBL) ambao ndio wasambazaji wa Guinness nchini Tanzania, watatumia uzoefu wao katika masoko, matangazo yenye ubunifu, na umaarufu wao katika kudhamini michezo mikubwa ya kimataifa kutoa burudani ya kipekee kwa mashabiki wa EPL msimu huu.
Msisimko wa wiki ya pili ya EPL utaanza kwa Brighton, ambao wanaongoza ligi hiyo, kukipiga na Manchester United katika uwanja wa American Express saa 8:30 mchana, zikifuatiwa na mechi nyingine sita. Ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City watakipiga na Ipswich Town saa 11:00 jioni na vijana wa Unai Emery wakiwakaribisha washika mitutu wa London, Arsenal majira ya saa 1:30 jioni. Guinness ina mpango wa kushirikiana na bar mbalimbali na maduka ya vilevi nchini kuhakikisha mashabiki wanapata burudani ya kutosha msimu huu nchini Tanzania. Mechi za Jumamosi hii zitaoneshwa mubashara maeneo yafuatayo. Warehouse Masaki, Happipola Masaki, Target Mbezi Beach, Rafikiz Mbezi Beach, Break Point, Amsterdam Mbezi Beach, Ice Liquor Land, na Waterfront.
Wankyo Marando, Meneja wa Chapa ya Guinness, alisema, “Kupitia uzoefu huu, tunataka kuonesha mchango wetu na kuinua burudani ya soka nchini Tanzania, ndani na nje ya uwanja, huku tukidumisha uhusiano mzuri kati ya Guiness, wateja wake na mashabiki, na wapenzi wa EPL kote ulimwenguni.”