Mwanamuziki wa muda mrefu kutoka nchi Colombia Shakira ambaye mwaka huu aliuanza kwa kuachia album yake mpya ambayo iliambatana na ziara yake ya muziki baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu .
Kulingana na Maisha na matukio mbali mbali ambayo amekutana nayo Shakira alipokuwa akifanya mahojiano na chanzo kimoja cha Habari nchini marekani Shakira aliulizwa kipi kinaumuhimu kwake kati ya mapenzi na urafiki na bila kujali alikiri kuwa “urafiki kwangu una umuhimu sana kwani nimepitia changamoto za aina mbali mbali katika Maisha yangu lakini nikiangalia asilimia kubwa ya watu ambao wamefanikiwa kuwa na mimi kwa kipindi chote niwapo katika magumu ni marafiki wamenizunguka,simaanishi sitaki mapenzi bali urafiki unadumu Zaidi kuliko mapenzi japo sina uhakika kama nitapenda tena lakini ikitokea sawa”
Alisema Shakira ambaye march mwaka huu aliachia album yake iitwayo Las Mujeres Ya No Lloran ikiwa ni album yake ya 12 tangu aanze kuutumikia ulimwengu wa burudani duniani.
Licha ya kuwa album yake ambayo ni ya 12 imekuwa album ambayo ameiachia baada ya kukaa kimya kwa muda wa miaka 7.