Kiri records ni moja kati ya lebo ya muziki nchini Tanzania ambayo imekuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza Sanaa ya muziki Tanzania katika kutoa vipaji vingi tofauti tofauti hasa kwa waimbaji wa muziki wa miondoko ya hiphop.
Licha ya lebo hiyo kuwa na wasanii wake lakini pia wamekuwa wakifanya kazi na wasanii mbali mbali kutoka Tanzania nan je ya Tanzania katika kazi mbali mbali,vile vile lebo hiyo imekuwa na utaratibu wa kufanya kazi zake binafsi ambazo ni za lebo hiyo na kushirikisha wasanii tofauti tofuti na mwka huu walifanya kazi kadhaa kama freestyle iliyofanywa na mkorinto,kudadeki iliyofanywa na tannah Pamoja na bando na sasa wameachia kazi nyingine iliyopewa jina la “dakika moja “ ikiwa imeshirikisha wasanii wanne ambayo ni platform,maarifa,salmin swag Pamoja na mwanadada tannah.
Kazi hii inapatikana katika vyanzo vyote vya kupakua na kusikiliza muziki .