Furaha ya wengi ilitoweka wakati watu wachache tu waliruhusiwa kuvuka mpaka wa Gatuna/Katuna, ambao ulipangwa kufunguliwa tena Jumatatu.
Kwa sababu ya mzozo wa kisiasa mamlaka nchini Rwanda ziliamua, mapema 2019, kufunga mpaka wake wenye shughuli nyingi zaidi na Uganda na kuwakataza watu kuvuka.
Wiki iliyopita, Rwanda iliamua kufungua mpaka huo siku chache baada ya Rais Museveni wa Uganda kumtuma mashauri wake, jenerali wa jeshi na mwanawe wa kiume kukutana na Rais Kagame,baada ya wajumbe na mikutano mingine kadhaa.
Tangu kufungwa kwa mipaka zaidi ya watu kumi, wakiwemo wanawake wawili, wameuawa kwa kupigwa risasi na vyombo vya usalama vya Rwanda "kwa kujaribu kuingiza bidhaa nchini kigendo".
Mamlaka ya Rwanda imesema waathiriwa walipigwa risasi ‘wakipambana na maafisa wa usalama’ au ‘kutoroka kukamatwa’.
Waganda na Wanyarwanda walifurahishwa na hatua hiyo na shughuli nyingi zilitarajiwa Jumatatu mpakani.
Chris Baryomunsi, waziri wa mawasiliano wa Uganda alisema kwamba“hajui sababu” kwa nini watu hawakuvuka kama ilivyotarajiwa.
“Kwa sababu nchi zote mbili zilikubali kufungua mipaka yao, kwa hivyo
tulitarajia shughuli nyingi”.
Mamlaka ya Rwanda ililaumu itifaki za Covid, lakini afisa mkuu ambaye hakutaka kutambulishwa "kuna mambo machache yanastahili kukamilishwa na Uganda kabla ya Wanyarwanda kuruhusiwa kuvuka".
"Suala lolote watakaloibua tutalazimika kulitatua ili kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ndugu.", Bw Baryomunsi alisema kuhusu masuala ambayo hayajatatuliwa.
Matukio
ya Jumatatumpakani yanaonesha kuwa “ingawa hatua kubwa imepigwa kutatua
mzozo, huenda bado haujamalizika”, Jean Paul Mugabo ambaye alishindwa
kuvuka kwenda upande wa Uganda.
Nchini Uganda, Rhoda Ahimbisibwe ambaye mumewe Sidney Muhereza aliuawa kwa kupigwa risasi kando ya mpaka wa Rwanda mnamo Juni 2020 anaoma mamlaka kuridhina.
"Sisi ni watu wamoja…Sisi watu wa kawaida tunahitaji kufanya kazi pamoja tena.",