Freeman Mbowe Akamatwa Songwe Airport Leo

Polisi Mkoani Mbeya wamemkamata Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA ( BAVICHA), John Pambalu muda mfupi baada ya wawili hao kuwasili Songwe Airport leo August 12,2024.


Mbowe amekamatwa baada ya kutua Songwe Airport kwa lengo la kufika Jijini Mbeya ili kufuatilia hatima ya Viongozi waliokamatwa jana August 11,2024 katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU).


Lissu, Mnyika na Sugu waliwasili Mbeya jana ili kuungana na Vijana wa Chama hicho kupitia Baraza la Vijana CHADEMA ( BAVICHA) waliokuwa wameandaa maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani leo Jijini Mbeya lakini baadaye walikamatwa.


John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje - CHADEMA, amethibitisha kukamatwa kwa Mbowe na Pambalu ambapo amesema “Mbowe na John Pambalu walipofika uwanja wa ndege Songwe leo wamekamatwa na Jeshi la Polisi, ukamataji huu umeongozwa na RPC wa Mbeya, tutaendelea kuwapa taarifa kadiri tunavyozipata “

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii