BAADA YA ONANA KUONDOKA SIMBA NA TIMU YAKE MPYA NI HII

WINGA wa Simba Mwenye Udambwi Udambwi  Willy Onana, licha ya kulamba mkwanja mrefu akijiunga na Muaither SC ya Qatar msimu ujao, atacheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya timu hiyo kushuka daraja.

Inaelezwa kuwa, Onana ameuzwa na Simba kwa dau la Dola 100,000 (zaidi ya Sh 250 Milioni), huku yeye akilamba Dola 150,000 (zaidi ya Sh 300 milioni) kwa kujiunga na timu hiyo ambayo msimu ulioisha imemaliza ya mwisho kwenye msimamo.

Muaither msimu ulioisha katika timu 12 zilizoshiriki Ligi nchini humo ilikuwa nafasi ya mwisho baada ya kukusanya pointi 14 kupitia mechi 22 ilizocheza ikishinda tatu, sare tano na kufungwa mechi 14.

Onana ametimka Simba baada ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja akijiunga nayo akitokea  Rayon Sports ya Rwanda akiwa mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo (MVP).

Biashara ya winga huyo imefanyika siku chache baada ya Simba kuamua kusajili kipa mwingine wa kigeni baada ya Ayoub Lakred kuumia akiwa mazoezini hiyo ujio wa Moussa Camara ‘Spider’ umemfanya winga huyo kung’oka Msimbazi baada ya taarifa kuvunja ni yeye ndiye anayempisha kipa huyo.

Kuondoka ndani ya kikosi cha Simba winga huyo ameungana na nyota wengine, Clatous Chama, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Babacar Sarr, Kennedy Juma, Israel Mwenda, John Bocco na Saido Ntibazonkiza waliotimikia timu nyingine katika dirisha hili la usajili litakalofungwa Agosti 15.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii