• Jumatatu , Januari 20 , 2025

100 wafariki kwenye maandamano, Jeshi latoa kauli

Takriban watu 100 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika maandamano dhidi ya Serikali nchini Bangladesh ya kumshinikiza Waziri Mkuu, Sheikh Hasina ajiuzulu.

Vyombo vya Habari nchini humo vimeripoti kuwa kati ya watu hao waliofariki wamo maafisa wa polisi 14, huku Jeshi la nchi hiyo likitangaza amri ya kutotoka nje kwa muda usiojulikana.

Maandamano hayo ya Agosti 4, 2024 yamechagizwa na yale ya mwezi uliopita yaliyoanzishwa na Wanafunzi wakitaka kusitishwa kwa mfumo wa ajira Serikalini wanaodai ulikuwa na upendeleo.

Serikali imetangaza mapumziko ya umma ya siku tatu kuanzia leo Jumatatu hadi Jumatano, huku huduma ya mawasiliano ya simu na mitandao ya kijamii zikizimwa na tayari watu 11,000 wakikamatwa kuhusiana na ghasia hizo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii