Maafisa 2 wa DCI Wakamatwa kwa Madai ya Kumuibia Mwanamume KSh 2m

Maafisa wawili wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wametiwa mbaroni kufuatia kisa cha wizi katika eneo la Kasarani. 

Kulingana na ripoti iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Kasarani chini ya OB 22/20/10/25, maafisa wawili wanadaiwa kumwibia Peter Gilbert Karitu usiku wa Jumapili, Oktoba 19, katika Hifadhi ya Mirema. 

Washukiwa watatu waliokuwa na bunduki aina ya AK-47 wanadaiwa kumdhulumu mwathiriwa saa 8.45 usiku alipokuwa akiegesha gari lake nje ya makazi yake. 

Mwathiriwa alilazimishwa kuingia nyumbani kwake na kuamriwa afungue sefu yake, iliyokuwa na hati za kusafiria na USD 16,000 (KSh 2,060,000) pesa taslimu. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii