Zaidi ya watu 40 wafariki dunia baada ya mabasi kugongana Uganda

Mamlaka za Uganda zinasema idadi ya waliofariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye Barabara Kuu ya Kampala–Gulu 46, kufuatia taarifa mpya kutoka kwa maafisa wa hospitali.

Maafisa wanasema baadhi ya waathiriwa waliodhaniwa kuwa wamekufa hapo awali walipatikana wakiwa wamezira na sasa wanapokea matibabu.

Wafanya kazi wa kutoa huduma za dharura wanashirikiana na maafisa wa afya kuthibitisha idadi hiyo na kutoa taarifa sahihi huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha mkasa huo.

Ajali hiyo iliyotokea Jumatano asubuhi,katika Kijiji cha Kitaleba, ilihusisha mabasi mawili, Lori na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser, kwa mujibu wa ripoti ya awali ya polisi.

Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka kutokana na baadhi ya abiria kujeruhiwa vibaya.

“Inaelezwa kuwa basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa likilipita lori na basi jingine lililokuwa likielekea Kampala lilikuwa likiipita gari ndogo ya Toyota Land Cruiser, lakini lilishindwa kufanya hivyo kwani tayari basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa limekaribia’’. Taarifa ya polisi imeeleza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii