Kuelekea msimu ujao Simba mpya yazidi kupikwa

Raisi wa Heshima na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba bilionea Mohammed Dewji ametangaza kamati mpya ya mashindano kuelekea msimu mpya wa 2024/25.  Mohammed Dewji ameendelea kuboresha safu mbalimbali za timu hiyo ili kurejesha heshima waliyoipoteza kwa misimu mitatu mfululizo.

Siku chache zilizopita raisi huyo alimtambulisha bw.Uwayezu Francois Regis kuwa mkurugenzi mtendaji wa Simba akichukua nafasi ya Imani Kajula anayekwenda kustaafu mwishoni mwa mwezi Agosti. Huu ni mwendelezo wa maboresho ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuvunja benchi la ufundi ,kusajili wachezaji vijana wenye uwezo na kuleta kocha wa viwango vya juu pamoja na benchi lake la ufundi ni ishara tosha kwamba mwekezaji huyo anataka kuiona Simba ya ndoto zake.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Agosti 1, 2024 imebainisha Wajumbe hao walioteuliwa ambao ni Mohamed Nassor, Azan Said, Richard Mwalwiba, Nicky Magarinza, Juma Pinto, Farid Nahdi na Farouk Baghozah.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii