Kituo cha Huduma za Hali ya Hewa cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) (CSC) kimeonya juu ya mvua kubwa ambayo inaweza kusababishwa na kimbunga inayokuja, iitwayo Batsirai.
CSC ilisema Batsirai anaibuka kutoka kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi.
Nchi za ukanda huo ambazo huenda zikaathirika ni Malawi, Namibia, Tanzania, Angola, Afrika Kusini, Botswana na Zimbabwe.
Onyo hilo limetolewa siku chache tu baada ya kimbunga Ana kuua makumi ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo.
Afisa wa Umoja wa Mataifa alisema kimbunga hicho kibaya kilionyesha uhalisia wa mgogoro wa hali ya hewa.