Saudi Arabia yalaani mashambulio ya anga ya Israel, Rafah

Saudi Arabia imelaani mashambulio ya anga yaliyofanywa na Israel mjini Rafah. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema serikali inalaani mauaji ya halaiki yanayofanywa na vikosi vya Israel kwa Wapalestina.

Riyadh imesema Israel inabeba dhamana kwa kinachotokea Rafah na kwenye maeneo yote inayoyakalia ya ardhi ya Wapalestina.

Kadhalika imesema hatua ya Israel ya kuendelea kukiuka maazimio ya kimataifa na kuhusu hali ya kibinadamu,inaongeza ukubwa wa janga linalowakabili Wapalestina.

Wakati huohuo jeshi la Israel imesema wanajeshi wake watatu wameuliwa katika mapigano Kusini mwa Gaza leo Jumatano,wakati likiendelea na operesheni yake Rafah.


Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo hilo.Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na Israel kuhusu tukio hilo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii