Diamond Platnumz na Zuchu wamethibitisha kuwa mapenzi yao bado yana nguvu baada ya kushiriki vipande vya wimbo wao mpya unaotarajiwa.
Zuchu, wiki moja iliyopita, aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kumkashifu Diamond baada ya kumpandisha jukwaani mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sarah, ambaye alisema ndiye aliyemshawishi kuimba wimbo uliomtambulisha.
Hii baadaye iliwafanya mashabiki kueleza kuwa Diamond huenda akamalizana na Sarah kwa sababu alikuwepo kabla hajaingia kwenye showbiz, jambo ambalo halikumfurahisha Zuchu.