Zirkzee kwenye rada za Arsenal

Klabu ya Arsenal inahusishwa na mpango wa kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi na Klabu ya Bologna ya Italia Joshua Orobosa Zirkzee.

Siri ya mpango wa usajili wa Mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 223 imefichuliwa na Mwandishi wa Habari za Sky Italia Gianluca di Marzio, akiamini endapo usajili huo utafanikiwa, Arsenal watalamba dume.

Marzio amesema anafahamu kuwa Zirkzee yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kusajiliwa huko Emirates Stadium kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya England na Michuano ya Kimataifa.

Hata hivyo Mwandizhi huyoa meonyesha wasiwasi kuwa huenda Zirkizee akapata changamoto ya kushindanishwa na Washambuliaji wengine ambao watapendekezwa kusajiliwa klabuni hapo, katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya Kiangazi.

Marzio amesema: “Kwa jinsi Arsenal wanavyocheza, nadhani Joshua Zirkzee anaweza kuwa msaada mkubwa kwao. Najua yuko kwenye orodha yao, lakini sijui kama yeye ndiye kipaumbele,”

“Pia yuko kwenye rada za Juventus na Milan, na kwa sasa yeye ndiye Mshambuliaji chipukizi anayefaa kwa wote.”

“Lakini Zirkzee ana hali ya kushangaza katika mkataba wake, kwani Bayern wana chaguo la kumnunua tena kwa euro milioni 40, lakini ikiwa Bologna itamuuza kwa vilabu vingine, watapata asilimia 60 tu ya ada ya uhamisho.”

“Inategemea kama Bayern wataamua kumnunua tena au la. Inategemea nani ataamua kumuuza Bayern au Bologna. Kwa hivyo ni hali ngumu katika suala hili.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii