Kocha wa Man United Ten Hag Ajipa Moyo "Mbona Man United Tamu tu Tupo Vizuri"

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amedai Manchester United ipo katika nafasi nzuri zaidi ya ilivyokuwa miezi 12 iliyopita, licha ya kuwa katika hatari ya kumaliza msimu bila taji lolote.


Man United ilikuwa ikitarajia kufuzu Europa kwa kushinda mechi yao ya mwisho na kuziombea mabaya Chelsea na Newcastle lakini mbali ya njia hiyo, pia wana nafasi ya kufuzu Europa League ikiwa watashinda mchezo wao wa fainali ya FA Cup dhidi ya Manchester City.


Ten Hag, ambaye hatma yake bado haijulikani baada ya Man Unite kufanya vibaya msimu huu, anaeleza ujio wa tajiri mpya pamoja na ongezeko la wachezaji wengi vijana katika kikosi cha kwanza vimeifanya timu hiyo kuwa katika mazingira mazuri tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita na walichukua Kombe la Carabao na kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi.


“Ukiangalia matokeo ni kweli utakataa maneno yangu, lakini kwangu mimi msimu huu tumefanikiwa zaidi, kwanza tuna wachezaji wengi vijana ambao wana ubora wa hali ya juu ambao siku hadi siku wanaimarika na wanaweza kuifanya timu yetu iwe katika viwango vikubwa vya ushindani siku za usoni.”


“Pia wanasaidiwa na baadhi ya wachezaji wenye uzoefu ambao kwa pamoja wanajenga timu nzuri yenye ushindani,” alisema Ten Hag.


Kocha huyu pia alifichua msimu ujao kutakuwa na maboresho makubwa kwa wachezaji licha ya ripoti kudai huenda wasisajili wachezaji wazuri kwa kushindwa kwao kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa.


“Kila mchezaji anavutiwa na kucheza Man United, mchezaji yoyote anayehitaji kucheza levo za juu lazima atakubali kujiunga na timu kama hii.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii