Ligi ya Afrika Kusini inafanya vyema na ni moja kati ya ligi bora barani Afrika lakini Sielewi kwanini timu yao ya taifa sio nzuri ”
“Wasimamizi wanatakiwa kukaa na kujadili kuhusu kuivusha timu hii ya taifa kwenda ngazi nyingine na kuifanya kuwa timu bora ya taifa barani Afrika au duniani. Naamini hilo linawezekana kwa sababu wana ligi bora”
Baada ya kuisikiliza hii interview imenijia picha ya hapa Nyumbani , sisi pia tuna Ligi bora sana lakini timu yetu ya Taifa haisadifu ubora wa Ligi yetu.
Wakati SA wanajitafakari ,Nafikiri wasimamizi wa mpira wetu pia wanatakiwa kufanya home work yao ili Timu yetu ya Taifa iwe tishio zaidi ya ilivyo sasa.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii