DRC: MONUSCO kufunga rasmi ofisi yake mjini Bukavu

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, inafunga rasmi ofisi yake leo Jumanne, Juni 25, huko Bukavu katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa nchi.


Bi Bintou Keita, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na ujumbe wa mamlaka ya Kongo wanatarajiwa kwa ajili hilo katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini asubuhi ya leo.

Sherehe ya kufunga imepangwa katika uwanja wa ndege wa Kazimu, katika eneo la Kabare, kulingana na Radio OKAPI.

Kufungwa rasmi kwa ofisi ya MONUSCO mkoani Kivu Kusini kunafuatia mchakato ulioanzishwa mwezi Januari mwaka huu wa kuondoka kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika mkoa huu.

Kuondoka kwa wanajeshi hao ni uamuzi uliochukuliwa mwezi Desemba mwaka uliyopita katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, baada ya majadiliano na Serikali ya Kongo.

Tangu wakati huo, kambi kadhaa za MONUSCO zilifungwa, zikiwemo zile za Kamanyola, Bunyakiri, Amsar, Baraka, Kavumba.

Tayari tarehe 30 Aprili, shughuli zote ndani ya mfumo wa mamlaka ya MONUSCO zilikuwa zimesitishwaa, huku jukumu la ulinzi wa raia sasa likiwa chini ya mamlaka ya Kongo.

Zaidi ya miaka 20 baada ya kutumwa kwa mara ya kwanza, askari wa Umoja wa Mataifa waliondoka katika mkoa wa Kivu Kusini baada ya MONUSCO kutoa misaada ya aina tofauti za vifaa kwa mamlaka ya Kongo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii