Vanessa Kashera Afunguka Mobetto Kuvunja Penzi Lake na Aziz Ki

Msanii wa Filamu za kibongo, Vanessa Kashera maarufu 'Vee Kashera' ameibuka na kudai kwamba mwanamitindo Hamisa Mobetto hawezi kuvunja mahusiano yake na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki sababu kila mtu ana nafasi yake kwa mchezaji huyo.


Vee Kashera amesema Aziz Ki ni mtu wake wa karibu na mahusiano yao ni urafiki na sio kama watu wanavyosema juu ya kiungo huyo kuwa wako kwenye mahusiano ya kimapenzi.


"Mashabiki ndio wanaozusha kuwa sisi ni wapenzi wakati hakuna sehemu tuliyoweka wazi jambo hilo. Hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi yangu kwa Aziz Ki kwa sababu kila mtu ana urafiki wake kwa nafasi yake, nina muda wangu kwa Aziz Ki na Hamisa atakuwa na muda wake." Amesema mrembo huyo


Kuhusu kwenda uwanja wa Benjamini Mkapa siku ambayo Yanga walikabidhiwa kombe, amesema hakujisikia kwenda kwenye sherehe za timu hiyo kukabidhiwa ubingwa sababu alikuwa na mambo yake mengine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii