WAKATI wabunge wakiendelea kusikiliza hoja za watia nia wanaowania kurithi mikoba ya Job Ndugai, Bungeni jijini Dodoma, Ndonge Said Ndonge, kutoka Chama cha AAFP huenda akawa ni mtia nia pekee alieibuka na kitita kutoka kwa wabunge waliokuwa wakimsikiliza kwa namna alivyo weza kujenga hoja na jinsi serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepiga hatua kuinua jamii na uchumi wa taifa katika kipindi kifupi.
Akiomba ridhaa kwa wabunge, Donge alisema yeye hapendi kuitwa Mgombea kwa sababu falsafa hiyo humaanisha kuna ugomvi.
“Natumia fursa hii kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania. Vijana sasa hivi wanasema anaupiga mwingi kwa sababu kaupiga mwigi sana kwenye madarasa,” amesema.
“Zamani kulikuwa na chaguzi karibu nne za kwenda form one. Wakati mwingine ushaozesha unaletewa barua kachaguliwa huyo awamu ya tatu mwisho wa siku aliyeozesha anauliza vipi huyo kesha pata ujauzito. Bado, basi huku kimeumana amefaulu,” amesema nakuongeza kuwa wakati huo wazazi walikuwa wakihoji fomu ya shule ananunua nani wazazi ama meme