Producer S2Kizzy Amjibu Baddest 47 Kuhusu Rayvanny Kumuibia Wimbo wa Sensema

Mtaarishaji wa muziki kutoka Bongo @s2kizzy amemjibu Msanii @badest_47 kuhusu madai ya kuwa ameibiwa Idea ya wimbo wa #Sensema ulioachiwa usiku wa kuamkia leo na Mastaa @rayvanny na @harmonize_tz
.
Baada ya ngoma hiyo kutangazwa kutoka Msanii #Badest aliibuka na kudai kuwa ameibiwa ngoma hiyo na hakuna taarifa aliopewa, #S2kizzy akifanyiwa Mahojiano na #XXL ya #CloudsFm amesema kuwa yeye ndio alioandaa wimbo huo na alimtumia #Badest.

"Mimi nahisi ni Misscomminication ambazo zimetokea, Mimi ndio nilitengeneza Beat na nilikuwa na Chorus tayari na nilimtumia #Badest na #Rayvanny na wote walipenda na #Rayvanny ndio alikuwa wa kwanza kuingiza mistari yake badae alifanya #Harmonize , #Badest yeye alichelewa tu hivyo hakuna mtu aliemuibia"

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii