Mabadiliko mapya ndani ya mtandao wa YouTube

Kwa mwaka 2023 ilifanikiwa kutengeneza watumiaji hai zaidi ya Bilioni 2.7 na kuifanya kuwa moja kati ya jukwa la mtandaoni lililotembelewa zaidi na watu wengi.


Tunafahamu kila mmoja wetu yuko na matumizi tofauti kuhusiana na YouTube, wakati wewe ukitumia kutazama maudhui yupo ambaye anatumia kupakia maudhui.

Sasa kama uko kwenye nafasi ya huyu mtumiaji huyu wa pili wa mtandao wa YouTube basi hii inakuhusu moja kwa moja

Thumbnail tatu ''3'' kwenye video moja. (Thumbnail Test & Compare)
YouTube kwa sasa wanafanya majaribio ya kumruhusu mtengeneza maudhui kupitia mtandao huo kuweka ''thumbnail'' zaidi ya moja. Hilo neno thumbnail lisikuchoshe sana kulielewa ni jalada la juu linaloonekana kwenye video husika kabla hujaitazama.

Ilivyo mpakia maudhui kwenye mtandao huo kwa sasa anaruhusiwa kuweka thumbnail moja pekee kwenye video yake, lakini kwa sasa endapo njia hii ikikamilika mtumiaji wa mtandao huo atawezeshwa kuweka thumbnail tatu kwa pamoja kwenye video moja alafu kwenye mzunguko wa ile video thumbnail zile zitakuwa zikibadilika alafu ile ambayo ilifanya vizuri zaidi kwa maana ya kuvutia watazamaji itaonekana kwako kama thumbnail iliyoshinda na utapewa nafasi ya kuchagua kuitumia moja kwa moja kama thumbnail rasmi ya video yako.

(a) ikiwa kama utachagua kipengele cha ''Thumbnail Test & Compare'' wakati unapakia video yako kwenye mtandao huo utawezeshwa kuweka Thumbnail '3' kwa pamoja na muda wa majaribio yake ni kwa muda wa saa moja hadi wiki, baada ya hapo iliyofanya vizuri unaichagua kwa ajili ya matumizi. Ikitokea hakuna iliyoshinda kati ya zote tatu ulizoweka basi ile ya kwanza itachaguliwa kama Thumbnail rasmi.

(b) Thumbnails utakazoweka hakikisha zinafuata sheria na taratibu zilizowekwa na YouTube na pia, utaratibu huu hautahusisha maudhui yanayotengenezwa kwa ajili ya watoto, Live video na maudhui ya watu wazima.

Nb: Thumbnail nzuri ndiyo sababu kubwa ya kuvutia watazamaji kwenye video yako hivyo hakikisha haukosei kwenye utengenezaji wa Thumbnail itakayovutia watazamaji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii