Kibwana Anahesabu Siku Yanga

BEKI kiraka wa Yanga, Kibwana Shomari na mwenzake Abdallah Shaibu ‘Ninja’, wanahesabu siku tu
za kurudi uwanjani mara
baada ya kupona majeraha yao.


Kibwana anayemudu
kucheza beki wa kulia na kushoto, wiki mbili zilizopita alikwenda Tunisia sambamba
na Ninja kwa ajili ya kufanyiwa
operesheni ya majeraha yanayowasumbua.


Kurejea kwa mabeki hao
kutampa upana wa kikosi Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra na kuthibitishwa na daktari wa timu hiyo, Youssef Ammar, mabeki hao watarejea uwanjani mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Februari 5, mwaka huu.


Ammar alisema mabeki hao
wataanza kufanya mazoezi mepesi ya uwanjani baada ya kumaliza program ya gym wanayoendelea nayo hivi sasa.


“Kibwana na Ninja
walifanyiwa operesheni ndogo ya goti ambayo itawarejesha haraka uwanjani tofauti na
Yacouba (Songne) ambaye
operesheni yake ilikuwa kubwa na kumfanya kukaa nje karibia miezi minne.
“Hivyo Kibwana na Ninja upo
uwezekano wa kujiunga na mazoezi ya uwanjani pamoja na wachezaji wenzake hivi
karibuni,”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii