Nick Cannon akatia Korodani zake Bima ya Bilioni 26

Muigizaji na mtangazaji wa TV maarufu nchini Marekani, Nick Cannon ameweka bima ya Korodani zake $10 Milion sawa na Bilioni 26 za kitanzania.

Cannon ameamua kufanya hivyo baada ya kutimiza idadi ya watoto 12 aliozaa na wanawake sita tofauti.

Gazeti la Daily Mail limeripoti muigizaji huyo aliishirikisha kampuni ya uuzaji wa bidhaa za kiume (DR. SQUATCH) ambayo ilifanyia tathimini korodani hizo kabla ya kuzikatia Bima.

Kwenye taarifa yake Nick alisema “Wanaochukia wanasema ni wakati wa mimi kuacha kuendelea kuzaa, lakini nimeamua kuongeza maradufu thamani ya korodani zangu na watoto wangu wa baadae.

Pongezi kwa Dr. Squatch kwa kuzipa Korodani zangu sifa inayostahili na kuniunganisha na ulinzi ninaohitaji ili kuendeleza mti wa Familia

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii