Rais Zelensky amewahotubia wabunge nchini Ufaransa akitoa wito wa silaha zaidi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewahotubia wabunge nchini Ufaransa na kutaka mataifa ya Magharibi kuipa msaada zaidi ili kushinda uvamizi wa Urusi kwenye nchi yake.
Imechapishwa:
Kiongozi huyo wa Ukraine pia amesema ana matumaini kuwa kongamano la amani kuhusu nchi yake, litakofanyika wiki ijayo nchini Uswizi, litasaidia kumalizika kwa vita vinavyoendelea.
Aidha, ameyataka mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Ufaransa, kufanya zaidi ili kuisaidia Ukraine kupata amani itakayodumu, huku akionya kuwa kinachoendelea kinaashirikia kuwa Ulaya sio bara la amani tena.
Tangu Urusi ilipoivamoia Ukraine Februari mwaka 2022, Zelensky amekuwa akitoa wito kwa nchi za Ulaya na Marekani kutoa msaada zaidia ya kifedha na silaha, hasa wakati huu ikiripotiwa kuwa vikosi vya Urusi vimekuwa vikisonga mbele na kuchukua maeneo zaidi ndani ya nchi yake.
Rais Emmanuel Macron siku ya Alhamisi alisema, nchi yake itatoa msaada wa ndege za kivita aina ya Mirage 2000 kwenda Ukraine, na kuwapa mafunzo marubani wake, ikiwa ni ushirikiano mpya wa kijeshi.