Real Madrid watangaza kumsajili Kylian Mbappe

Winga wa Ufaransa, Kylian Mbappe amekamilisha taratibu zote za usajili za kujiunga na Real Madrid akitokea PSG.


Kwa mujibu wa ripoti, Mbappe atakuwa akilipwa mshahara wa €15m kwa mwaka sawa na Tshs Bilioni 42.4


Mbali na mshahara, Mbappe atalipwa bonasi ya usajili ya €100m sawa na Tshs Bilioni 283 ambayo kila mwaka atalipwa €20m (Tshs Bilioni 57) kwa kipindi cha miaka 5.


Taarifa hiyo imetolewa na Klabu ya Real Madrid ikiwa ni taarifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii