Msanii wa kizazi kipya kutoka Mwanza Tanzania Vanillah music ambaye kwa sasa ni msanii ambaye anasimamiwa chini uya lebo ya muziki maarufu kings music amefanikiwa kwa asilimia kubwa kufanya muziki wake vyema katika Nyanja tofauti na pia watanzania kumpokea vizuri tangu alipotambulishwa mwaka 2023.
Vanillah ambaye kwa sasa yupo jijini Mwanza kwaajili ya ziara yake katika vyombo mbali mbali vya Habari ameweka wazi kuhusu suala zima la muziki wake na namna anavyofanya usambazaji wa muziki wake kwa muendelezo wa “daladala tour” akifanya mahojiano kupitia jembe fm ndani ya kipindi cha Hitzone kinachoongozwa na Nattye brandy Pamoja na B forty five aliulizwa swali kuhusu kuonekana na d voice na kama kuna mpango wowote wa kufanya wimbo Pamoja licha ya kuwepo kwa sintofahamu kati ya lebo na viongozi wa lebo zao alijibu,
“ni kweli nilikutana na D voice ni msanii ambaye anafanya mziki mzuri lakini pia anasikiliza ngoma zangu sana kwa hiyo ni swala la muda tu kwenye kufanya kazi na sio D voice peke yake hata Ibraah bila kusahau Mbosso lakini ni mpaka makubaliano ya pande zote mbili yakikamilisha kila kitu kibiashara”
Alijibu vanilla ambaye licha ya kufanya muziki na kuandikia wasanii mbali mbali anaamini Zaidi katika heshima na kutokumchukulia mtu aliyemziki wa kawaida.