SITAKI KUWA NA WATOTO SASA KWA SABABU SIWEZI KUTOA UPENDO NILIOPATA KUTOKA KWA WAZAZI WANGU SASA - BURNA BOY

Mwimbaji nyota wa Nigeria, Burna Boy amesema hataki kuwa na watoto kwa sasa kwa sababu wakati huuhawezi kutoa mapenzi aliyoyapata kutoka kwa wazazi wake. 

Akizungumza na  mashabiki wake wakati wa kikao cha moja kwa moja kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Burna Boy alifichua zaidi kwamba "operesheni" yake ya sasa haitamruhusu kuwa na wakati wa watoto wake kama vile angependa. 

Aliongeza kuwa ataanza kupata watoto akiwa ametulia zaidi na anaweza kuwa pamoja nao kila siku. Burna pia alisema kuwa hata kama hawezi kupata watoto, sayansi imerahisisha kufanya hivyo.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii