MKUU wa Wilaya ya Songwe Simon
Simalenga amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara yenye kipande
cha urefu wa kilomita 7 kutoka Kata ya Kanga kwenda Kata ya Ifwenkenya
ambayo inajengwa na Mkandarasi Elimak Engineering CO. LTD na ujenzi
unaendelea vizuri.
Katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya ya Wilaya ya Songwe CPA Cecilia Kavishe, Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya, MENEJA wa TARURA MKOA wa Songwe Kaka Kilian
Haule, Meneja wa TARURA wilaya ya Songwe Eng. Yusuph Shabani, Kaimu DAS
Ndugu Chesko Mbilinyi na Viongozi wengine wa Wilaya.
Akizungumza
akiwa kwenye ziara hiyo Simalenga amesema kimsingi wananchi wa Wilaya
ya Songwe wamejawa na moyo wa shukrani kutokana na ongezeko la fedha za
Barabarabara kutoka Sh.milioni 640 walizokuwa wakipewa mpaka kufikia
Sh. Bilioni 2.84 katika kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita
chini ya Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan.
Aidha
amesema baada ya kazi ya ujenzi wa Mitaro unaendelea sasa, kazi
itakayofuata ni kumwaga kifusi kwa urefu huo wa kilomita 7 kisha
Mkandarasi atahamia Barabara ya Kata ya Galula, Chang’ombe mpaka Mbuyuni
yenye urefu wa kilomita 6.
“Mpaka sasa kazi imeshafanyika kwa
asilimia 25 ambapo Mkandarasi huyu anaendelea kutumia fedha zake.
Ikumbukwe kwa mujibu wa Mkataba kazi hii inatakiwa kukamilika ndani ya
miezi 8,"amesema Simalenga.