Idadi kubwa ya wapiga kura vijana katika uchaguzi wa rais Marekani wanasema wanatamani wangekuwa na mtu mwingine na siyo Joe Biden au Donald Trump kumchagua.
Lakini wapiga kura vijana wanamuunga mkono nani kati ya hao?
Kinyang’anyiro kati ya wagombea wawili watarajiwa wa zamani kutoka vyema viwili vikubwa kuwania urais, kuna maswali katika kampeni kuhusu afya ya wagombea katika kampeni hii kuhusu nguvu ya waombea kuwepo madarakani.
Hasa kutoka wapiga kura vijana. Deswmon Kager angependa kuwa na chaguo tofauti.
Desmond Kager, Mpiga Kura, New Hampshire anasema: “Kama Warepublican na Wademocrat, unajua, muweke mtu mwingine kwenye tiketi ya uraia, unafahamu, ni vizuri kupigia kura, halafu nitawapigia kura.”
Ukusanyaji maoni wa Pew Research wiki iliyopita umebaini kwamba theluthi mbili ya wapiga ni chini ya umri wa miaka 30 huenda watawaondoa wagombea wote wawili kama wakipata fursa hiyo. Kwahiyo ni vijana gani wanamuunga mkono Biden au Trump?
Wasi wasi kwamba haki ya uzazi ina maana Biden ana uungaji mkono wa Francesca Panniello.
Francesca Panniello, Mpiga Kura, New Hampshire anasema: “Nadhani kutoa mimba, kutoa mimba ni muhimu kwangu. Huduma katika utoaji mimba, haki ya kuwa na uwezo wa kuchagua.”
Haki ya utoaji mimba na bangi ya burudani yote yako katika kura mwezi huu wa Novemba. Hiyo ni kuwaita wapiga kura vijana kwa sababu za chama cha Democratic, anasema Jayden D”Onofrio.
Jayden D’Onofrio, Mpiga Kura, Florida anasema: “Wapiga kura vijana wana fursa ya kweli kubadili uwanja wa uchaguzi hapa Florida. Tumeona kwamba haki ya kufanya maamuzi na bangi ya burudani ni muhimu kwa imani na muhimu kwa wapiga kura vijana, na kilicho juu katika mawazo yao, hasa ni haki ya kufanya maamuzi.”
Baadhi ya vijana wanampinga Biden kwa uungaji mkono wake kwa Israel katika vita huko Gaza. Lakini huenda akampata mpiga kura Eliana Stein.
Eliana Stein, Mpiga Kura, Massachusetts alieleza:
“Nahisi kama hivi sasa, kwangu mimi, jambo moja muhimu sana ni kuendeleza uungaji mkono kwa Israel, hasa wakati wote wa mzozo ambao unaendelea. Kwahiyo, kwa kweli nashukuru kila kitu ambacho Rais Biden amefanya kuiunga mkono Israel katika mzozo wa sasa.”
Vijana wanaomuunga mkono Trump ni pamoja na wapiga wa Wisconsin Briauna Bonilla na Jonathan Boyer.
Briauna Bonilla, Mpiga Kura, Wisconsin: “Nina maana, nimejaribu kuwa na mawasiliano na watu ambao hawampendi Trump, na wanasema, “unaweza kuondoka. Sitaki kuongea na wewe tena.” Kwahiyo nadhani hilo ni tatizo kuu. Watu hawako wazi kusikiliza. Wanasema tu. ‘Kama unampenda Trump, wewe ni mtu mbaya au mambo kama hayo, nahisi hivyo.’
Jonathan Boyer, Mpiga Kura, Wisconsin: “Ndiyo, hakujawahi kuwa majadiliano yoyote ya wazi.”
Briauna Bonilla, Mpiga Kura, Wisconsin anasema: “Nahisi kama una uwezo wa kufungua majadiliano. Nahisi kama watu wengi wanafanikiwa, nasema, unajua, wanatokea kama hawawezi kusema kitu au hawataki kuzungumza nawe, au wanamwambia kila mtu.”
Wafuasi vijana wa Trump wamewazoea watu wa umri wao na kuhoji maamuzi yao ya kisiasa, anasem Isayah turner.
Isayah Turner, Mpiga Kura, Wisconsin anasema: “Kama, napenda kwenda baa nikiwa vimevaa kofia ya Trump 2024, naangaliwa kiajabu, kama sina akili kukiwepo watu, lakini haijalishi.”
Turner anasema anaupenda msimamo wa Trump dhidi ya rushwa.
Isayah Turner, Mpiga Kura, Wisconsin: “Nadhani kuna mambomengi ya kashfa ambayo yanaendelea kote duniani. Nadhani Trump ni mmoja wa wanaume ambao kwa hakika alikuwa na ujasiri wa kuyasema hayo, kuwaita watu hao na hakuwa na uoga, unajua hilo? nahisia kama atafanya vizuri kwa nchi, unafahamu?”
Ukusanyaji maoni ya Reuters na Ipsos mwezi Machi umewaonyesha Wamarekani kati ya umri wa miaka 18 na 29 wanampendelea Biden dhidi ya Trump kwa asilimia tatu. Hiyo ni idadi ndogo kuliko mwanya wa asilimia 24 ambao Biden alishinda kura ya vijana miaka minne iliyopita.