Wafungwa zaidi ya 400 wameachiwa Venezuela

Spika wa bunge la Venezuela Jorge Rodriguez amesema zaidi ya watu 400 wameachiliwa kutoka gerezani kama sehemu ya mchakato unaoendelea wa kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa.

Akizungmza siku ya Jumanne Rodriguez alisema uamuzi wa kuwaachilia baadhi ya wafungwa si wafungwa wa kisiasa, bali baadhi ya wanasiasa ambao walivunja sheria na kukiuka katiba, watu waliotaka uvamizi ulikubaliwa.

Rodriguez alisema wakati wa kikao cha bunge kuwa hatua hii ilikusudiwa kukuza na kuimarisha jamii kuishi kwa amani. Ingawa alisema zaidi ya watu 400 waliachiliwa hakutoa ratiba maalum.

Masharika ya kutetea haki za binadamu yanakadiria kuwa idadi ndogo ya wafungwa kati ya 60 na 70 wameachiliwa katika siku za hivi karibuni.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii