Denmark na Greenland zimeungana kupinga wito wa rais wa Marekani Donald Trump kutaka kukitwaa kisiwa cha Greenland hivyo viongozi wa nchi hizo wamesema wanaichagua Jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya badala ya Marekani.
Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari huko Copenhagen, Frederiksen alisema watasimama pamoja na raia wa Greenaland na wanaichagua Jamhuri ya Denmark, NATO na Umoja wa Ulaya badala ya Marekani.
Aidha viongozi hao wa Denmark na eneo la Greenland nchini humo siku ya Jumanne wameonesha mshikamano dhidi ya wito wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kutaka Marekani ikichukue kisiwa hicho cha kimkakati cha eneo la Aktiki usiku wa kuamkia mikutano muhimu huko Washington kuhusu suala hilo.
Mawaziri wakuu wa Denmark na Greenland walisisitiza kwamba eneo hilo ni sehemu ya Denmark, na hivyo liko chini ya mwavuli wa jumuiya ya kujihami ya NATO.
Hata hivyo katika makubaliano hayo Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen na Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen, walitaka kusisitiza mshikamano wao huku mawaziri wao wa mambo ya nje, Lars Løkke Rasmussen wa Denmark na Vivian Motzfeldt wa Greenland huku wakijiandaa kwa mazungumzo katika Ikulu ya White House leo Jumatano na makamu wa rais wa Marekani JD Vance na waziri wa mambo ya nje Marco Rubio.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime