Kutoka kushinda tuzo Kadhaa, Kutajwa katika Tuzo za Tanzania Music Awards TMA 2022, Tuzo za Kimaraifa Zikomo Awards 2023 Toka Nchini Zambia.Hadi kutajwa kwenye orodha za wasanii wa kufuatiliwa, safari ya Banny imekuwa ya mafanikio. EP zake mbili, “Banny Touch” na “Banny Vibes”, zimefungua milango na kuukaribisha ujio wa albamu yake.
Malkia ndio jina la albamu ya kwanza ya Banny, inayotarajiwa kuachiwa Oktoba 2024. Albamu hii inaashiria hatua muhimu katika kazi ya Banny, ikithibitisha ukuaji wake kama msanii na uwezo wake wa kuwa mmoja kati ya wanaochangia ukuaji wa muziki wa Tanzania. Kwa mujibu Tu ni kuwa “Malkia” italeta mkusanyiko wa nyimbo zenye nguvu kutoka kwa Banny na wa wasanii wengine wenye vipaji, ambao ameshirikiana nao.
Malkia inatazamiwa kuwa kazi ya kipekee, ikimkutanisha Banny na vipaji vya muziki vya hali ya juu. Kufanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara wa muziki ndio kipaumbele cha sasa katika kuhakikisha albamu hiyo nakamilika. Banny amejitolea kuhakikisha kuwa albamu hii inatambulishwa vyema kwa mashabiki wake na jamii yote ya Bongo Fleva.
Kwa kufuatilia safari ya Banny kwenye muziki, ni wazi kuwa albamu yake ya kwanza, “Malkia”, utakuwa mwanzo na sababu ya mafanikio yake ya baadae. Mashabiki wa muziki wanatarajia kupata uzoefu wa kipekee kutokea kwenye albamu hiyo, ikionyesha uwezo wa kipekee wa Banny kama mwanamuziki na msanii anayekuja kwa kasi yake. Kwa sasa Banny anaendelea kufanya kampeni ya usikilizwaji wa wimbo wake ‘Feel Fre’, aliomshirikisha Reime Schemes