RECAP: Hakuna Matata yazua Taharuki Uingereza

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumza namna Komasava ya Diamond na Hakuna Matata ya Marioo zinaisumbua Afrika.

Amesema kuwa kwa sasa muziki wa Amapiano ndio muziki Bora duniani sio tu Afrika, hata wasanii Davido na Burna boy wamefanya Remix ya Tswala Bam.

Kwa upande wa Afrika Tanzania inauwezekano mkubwa ikawa ndio taifa la pili kwa kuzalisha muziki mzuri wa AMAPIANO baada ya Afrika Kusini.

Muziki huu upo juu ya AFRO BEAT ya Nigeria kwa sasa, hivyo msanii akifanya Amapiano basi hufuatiliwa zaidi.

Anaongeza kuwa ukitaja nyimbo tano bora Afrika kwa sasa huwezi kuzitoa Komasava & Hakuna Matata, ukipita kwenye page ya mchezaji wa timu ya wanawake ya MANCHESTER UNITED amelitumia neno HAKUNA MATATA.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii