DJ Bella "ningewashirikisha Burna Boy, Kizz Daniel, Wizkid, Davido kwenye wimbo mmoja "

Mask Queen DJ Bella, mvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mbio ndefu zaidi za tamasha la moja kwa moja, ametangaza mipango ya kutengeneza wimbo mkali utakaowashirikisha mastaa wanne wakubwa wa muziki barani Afrika - Burna Boy, Wizkid, Kizz Daniel na Davido.

Ushirikiano unaotarajiwa sana unatazamiwa kuleta pamoja vipaji vya muziki vya wasanii hawa wanne katika mchanganyiko wa kipekee wa Afrobeats, Dancehall na Reggae.

 DJ Bella alionyesha kufurahishwa kwake na ndoto hii, akisema: “Siku zote nimekuwa shabiki wa muziki wao na athari ambayo wamekuwa nayo kwenye tasnia. Ninaamini kolabo hii itakuwa ya kubadilisha mchezo, sio kwangu tu bali hata kwa muziki wa Kiafrika kwa ujumla. Naomba tu ifanye kazi!”

"Itakuwa ndoto wakati nguzo hizi kali za tasnia zitakubali kuja pamoja ili kufanikisha hili. Wakati huo huo, nitadondosha mixtape nikiwashirikisha hao wanne; kuchanganya nyimbo zao maarufu katika mp3 moja”. Dj Bella aliahidi.

Mixtape hiyo inayotarajiwa kuachiwa miezi kadhaa ijayo, ni uthibitisho wa dhamira ya DJ Bella ya kuondoa vikwazo katika tasnia ya muziki. Akiwa DJ wa kike, amekumbana na changamoto nyingi katika nyanja inayotawaliwa na wanaume, lakini azimio lake na ustahimilivu umefanya atambuliwe sana.

"Nitafurahi zaidi kupata fursa ya kufanya kazi na wasanii wenye vipaji kama vile Burna, Kizz, David na Wiz," alisema DJ Bella. “Ninaamini kuwa muziki ni chombo chenye nguvu cha kuunganisha watu na kukuza mabadiliko chanya. Kwa ushirikiano huu, tunalenga kuunda wimbo ambao utawatia moyo na kuwainua wasikilizaji wetu.

"Ingawa Kizz Daniel amekuwa akidharauliwa kwa muda mrefu sana, ninaamini anastahili nafasi kama msanii bora wa Nigeria ambaye amewapa kila mtu Hits back to back. Kila wimbo alioutoa ulikuwa wa mbwembwe” Mbali na hawa watu, ninafanyia kazi nyimbo na video nyingine nyingi za muziki zenye vipaji vya hali ya juu kote Afrika”. Aliongeza.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii