Idadi ya vifo imeongezeka kufuatia kuanguka kwa jengo huko Afrika kusini

Watu 29 wameokolewa wakiwa hai hadi sasa. Timu za uokoaji zimekuwa zikifanya kazi bila kuchoka tangu wakati huo.

Idadi ya vifo kutokana na kuanguka kwa jengo moja nchini Afrika Kusini imepanda hadi 20, mamlaka za manispaa zimesema Jumapili, huku watu 32 wakiwa bado hawajulikani waliko kwa karibu wiki moja baada ya jengo hilo kuanguka.

Timu za uokoaji zimekuwa zikifanya kazi bila kuchoka tangu jengo hilo la ghorofa lililokuwa bado kwenye ujenzi kusini mwa mji wa George lilipoanguka Jumatatu mchana huku wafanyakazi 81 wakiwa kwenye eneo hilo.

Watu 29 wameokolewa wakiwa hai hadi sasa. Siku ya Jumamosi manusura ambao hawakutarajiwa walipatikana baada ya saa 116 kutoka chini ya vifusi vya jengo lililo-poromoka, mamlaka ya manispaa ilisema. Mamlaka za mkoa zilielezea tukio hilo kama miujiza, wakati wakikabiliana na muda katika juhudi za uokoaji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii