Mwamba anarudi tena nyumbani

Nyota wa Chelsea, Thiago Silva mwenye umri wa miaka 39 atajiunga tena na klabu ya Fluminese ya kwao Brazil.

Chelsea itamruhusu kujiunga na klabu hiyo ya Brazil mapema sana kuliko kawaida na ataruhusiwa kufanya mazoezi na Fluminese kabla ya Julai Mosi.

Kwa mujibu wa taarifa, Rais wa klabu ya Fluminense, Mário Bittencourt amevutiwa saa namna Chelsea ilivyohusika kuhakikisha, Thiago Silva anarejea kwenye klabu yao.

Rais huyo amependezewa na ukaribu wa Chelsea na ametangaza atakuwa shabiki wa Chelsea na amepanga zichezwe mechi mbili za kirafiki kati ya klabu hizo.

Mchezo mmoja utachezwa nchini Uingereza na mwingine Brazil kwenye dimba la klabu hiyo, dimba la Maracana mechi hizo zikiwa maalumu kwa ajili ya Thiago Silva.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii