KURA ZA SPIKA KUPIGWA LEO

 Bunge la Tanzania limeanza vikao vyake hii leo huko jijini Dodoma, ambapo limeanza shughuli zake kwa kuendesha uchaguzi wa spika mpya atakaeliongoza bunge hilo.

Nafasi ya spika iliachwa wazi pale, aliyekuwa spika wa bunge Job Ndugai kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Januari.

Jumla ya wagombea tisa kutoka vyama kadhaa vya kisiasa wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

Kati ya majina hayo, ni jina la mgombea mmoja tu ambae ndio mbunge huku wengine wakiwa sio wabunge.

Miongoni mwa vyama vilivyowasilisha majina, mbali na chama tawala cha CCM, vyama vyengine ni kama vile NRA, TLP, CCK, ADA TADEA, SAU, ADC, AAFP na DP.

Tayari wabunge 344 wa CCM ambão ndio wengi bungeni wamempigia chapuo kwa kura ya ndio mgombea wao ambae ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson.

Iwapo Dr. Tulia atapitishwa hii leo na kuchukua nafasi ya kuongoza muhimili huo wa bunge, basi atakuwa mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii